HARD MAD |
“Idea ilikuja kama hivi, kuna mshikaji mmoja amekuja kutoka Dar es salaam ambaye yeye ni mwana sana katika upande wa filamu…yeye ndio alinipa hiyo idea bwana blaza eeh mimi naitwa Yahaya naishi Kinondoni , sasa naona kama hii ngoma imenilenga nini nikamwambia hamna labda katika art tu ya mtu na nini na nini sababu wale Yahaya wanaoishi Kinondoni bado ni wengi”. Hard Mad alizungumza jana kupitia Showtime NewChapter ya Radio Free Africa, Mwanza na Renatus Kiluvia aka Bizzo.
Hard Mad aliendelea kusimulia kuwa baada ya Yahaya kumfuata alimwambia wimbo wa Jide umemsababishia awe na wakati mgumu kutokana na jinsi watu wanavyomchukulia sasa wakidhani anayeimbwa ni yeye kutokana na mambo mengi yaliyoimbwa yanamhusu moja kwa moja.
“Akaniambia ndio lakini inaniuma sana lakini mimi nilikuwa naishi na watu vizuri naendesha mandinga ndinga za watu wananiamini lakini saizi naona kila mtu ninaemfuata ananiambia we Yahaya tu unajua zile.” Alisema.
“Alivyokuja ndio akaniambia bwana blaza mi sio msanii lakini hii idea unaweza kuifanyia kitu flani kwasababu wewe ni msanii wa zamani na sikuwaza kama nitakutana na wewe studio kama hivi nilikuwa nakusikia tu kwenye radio na kukuona kwenye TV nashukuru nimekuona labda unaweza ukanifanyia kitu kuhusiana na hili ili roho yangu na mimi isuuzike.”
Hard Mad ameendelea kusema kuwa baada ya kupewa idea na Yahaya aliusikiliza vizuri wimbo na kujaribu kuanza kutengeneza jibu,
“Kwahiyo ndio hivyo idea ilivyokuja na mimi nikakaa nikaisikiliza nikajaribu kufanya kitu naona na kitu kikakua na pia katika upande mmoja au mwingine nikawa nimeona kama ni art pia kwasababu hata ukisikiliza miziki ya zamani ya kina Marijani Rajab, Msondo ukisikiliza Juwata Jazz kuna design flani walikuwa wanafanya ya music, kwamba huyu anaweza akatoa swali mwingine akajibu na ndo kitu ambacho kilikuwa kinafanya hasa ukue katika kiwango kikubwa sana hapa nchini.
Lakini sikuhizi naona hicho kitu kinaenda kinakufa hata watu wakijibu wanakuwa yani hata kama mtu ameuliza swali wengine wanaogopa kujibu wanaona kama watabeef, lakini mi nahisi sio kubeef ni kwamba unafanya sanaa inakuwa na changamoto.” Alisema Hard Mad.Ukiskiliza vizuri beat ya ‘Naishi Ghetto’ ni kama ile ile ya Yahaya lakini imepigwa upya, producer wa ‘Yahaya’ ya Anaconda, Man Walter wa Combination Sounds pia amezungumzia wimbo huo na kudai kuwa yeye hajahusishwa kwa namna yoyote katika kuombwa idhini ya kutumiwa kwa ubunifu wa kazi yake katika wimbo wa Hard Mad.
MAN WALTER |
“Mi naona kilichofanyika si sawa kwasababu hakukuwa na mawasiliano, unaweza ukapewa go ahead kwamba poa baada ya kusikiliza unataka kuimba nini lakini naweza nikakubali hayo yote sababu pengine ni namna ya mtu kutafuta namna ya kutoka, na wakati mwingine tukiwa tunazizungumzia mambo haya kama hivi ndio tunazidi kumpa mtu credit, lakini mi naona bigup apewe yule mtu ambaye alianzisha idea big up to Lady JayDee afu big up to Combination Sounds Kombinenga.” Aliongeza Man Maji wa Kombinenga
Walter amesema kuwa nyimbo kama hizo huwa ni za kiharakati tu na hazistahili kuchezwa kwenye radio bali zinafaa kusambazwa katika mitandao ya kijamii peke zaidi.
Man Water aliulizwa juu ya hatua anazopanga kuchukua baada ya kuusikia wimbo huo wa Hard Mad:
“Haya mambo ya haki miliki bado vitu vingi havijakaa sawasawa watu wengi sana wanauchezea muziki wanachezea pia kazi za watu wengi sana. Kwahili siwezi kusema chochote ni mapema sana kwasababu track nimeisikia leo, sijazungumza na Jide kama kuna taarifa zozote lakini ninauhakika kwasababu track haijatendewa haki kama vile iko chini ya kiwango sisemi kwa ubaya lakini ukizi compare unaweza ukaona mmoja anaeleweka anaongea nini mwingine haeleweki.”
Water ameonesha kutokuwa na tatizo na Hard Mad kwasababu wanafahamiana vizuri, isipokuwa amesisitiza kitu ambacho hakubaliani nacho ni kitendo cha kutopewa taarifa mapema na wahusika.
“Lakini pia Hardmad ni mwanangu hata hivyo nimeshangaa kwasababu Hard Mad kwanini asizungumze na mimi afu ni mshikaji wangu sana tena sio kitoto kiasi kwamba hata akisikia mimi nazungumza na yeye kupitia media kama hivi anaweza na yeye akashtuka kidogo lakini ni mtu ambaye tuko naye Kino tunaweza tukazungumza….tukatoa Baraka za ile go ahead ya kufanya anachokifikiria kufanya, lakini sivyo hivi alivyofanya sababu yeye kama ni msanii mkubwa sijui analeta picha gani kwa wasanii ambao wanachipukia wanaweza wakaona hii ndio njia sahihi ya kutoa track.”
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako