Monday 3 March 2014

MADHARA YA DAWA ZA HOSPITALINI



Madhara ya Matumizi ya dawa (side effects) kwa Bwana Hafidh Masokola Damson ambaye kwa sasa anaishi Tabora mjini eneo la National Housing amebadilika maeneo yote ya viungo vya mwili wake isipokuwa meno pekee na kuwa kama albino hata kufikia hatua ya kujiunga na chama cha Maalbino Tanzania tawi la Tabora.
Bw.Hafidh Masokola Damson ambaye alibadilika na kuwa Albino kutokana na matumizi ya dawa za Malaria baada ya kuzitumia mnamo mwaka 2010, Kwa maelezo yake mara baada ya kunywa dawa aina ya Metakelfin alianza kubabuka ngozi ya mwili wake huku magamba yakitoka mithili ya nyoka katika mwili wake.
Kwa mawasiliano yake unaweza kumsaidia kwa kumpigia kwa simu ya kiganjani 0767 298 348 au 0658 298 348.




No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako