Friday 28 March 2014

OMMY DIMPOZ AENDELEA KUFANYA KWELI



Ni zamu ya staa wa bongofleva anayetajwa kuwa wa pili kwa kupokea malipo makubwa kwenye show mbalimbali anazozifanya (milioni nane kwa show za ndani ya nchi).
Siku kadhaa baada ya kutua Tanzania akitokea Marekani na Uingereza alikokwenda kufanya show pia, Ommy Dimpoz amepata dili jingine zuri kwa kualikwa kuimba na band yake aliyotoka nayo bongo katika party ya kampuni ya mafuta huko Muscat Oman.
Kwa siku kadhaa Ommy ambae ni miongoni mwa vijana wachache wa bongofleva wanaosifika kwa kujituma na kuwa serious na kazi, alionekana akifanya mazoezi na band yake ambayo ndio atahusika nayo mwanzo mwisho kwenye stage Leo Ijumaa March 28 2014

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako