Thursday 20 March 2014

MESSI AVUNJA REKODI YA UFUNGAJI WA MAGOLI BARCELONA



Jumamosi iliyopita, Lionel Messi aliweka rekodi nyingine kubwa kwenye soka, dhidi ya Osasuna aliifikia na kuipita rekodi ya magoli ya gwji wa klabu ya FC Barcelona Paulino Alcantara, ambaye aliifungia Barca jumla ya mabao 369.

Messi aliivunja rekodi hiyo kwa kufikisha mabao 371, baada ya kupiga hat trick dhidi ya Osasuna, na katika kusherehekea rekodi hiyo – Messi aliamua kuvaa jezi ya Paulinho Alcantara pamoja na mpira – vifaa vya michezo ambavyo Alcantara alivitumia miaka ya 1920s.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako