Monday 24 March 2014

NDEGE YA MALAYSIA MH370 IMEPOTEA, HAKUNA ALIYEPONA


Shirika la ndege la Malaysia limewaambia jamaa na familia za abiria waliokuwa wanasafiri kwa ndege iliyotoweka MH370 kwamba ndege hiyo imepotea na kwamba hakuna manusura.
Tangazo hilo limetolewa kwa familia hizo kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi , ambao BBC iliweza kuuona.
Ndege ya Malaysia MH320 ilitoweka ikiwa na abiria 239 baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur tarehe 8 mwezi huu.
Aidha tangazo hilo limekuja huku juhudi za kutafuta mabaki ya ndege hiyo Kusini mwa Bara Hindi zikimalizika kwa siku ya tano bila mafaniko

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako