Thursday 27 March 2014

RAIS KENYATTA ASIMAMISHA MSAFARA WAKE NJIANI KUPATA CHAKULA CHA MCHANA



Vituko vya mara kwa mara haviishi kwa Raisi wa Kenya, Bwana Uhuru Kenyatta, ambapo wiki hii wakati alipotoka kwenye mkutano wake yeye na marais wengine aliamua kusimamisha msafara wake na kupata chakula cha mchana eneo la kawaida kabisa.
Tukio hilo limewashangaza wengi ambao walikuwa wakishangaa msafara huo wa Rais ukipita mara ghafla ukakata kona na kupaki pembeni na waheshimiwa kushuka kupata mlo wao wa mchana kwenye eneo liitwalo Kaijado tena chini ya mti.
Walioshuka kupata chakula cha mchana ni Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na naibu wake William Ruto pamoja na wasaidizi wao.
Rais Kenyatta anaonekana kuwa karibu na kutaka kuishi maisha ya kawaida tofauti na yale ya waheshimiwa maraisi wa nchi zingine, ambapo wiki iliyopita video moja ilimuonyesha akinunua karanga kwa muuzaji anayetembeza mtaani.
Hakuishia hapo pia aliwahi kutembea jijini Nairobi bila msafara kama ilivyozoeleka hadi Trafiki akamshangaa aliporuhusu gari za upande huo na kumuona akiwa anaendesha gari hizo ambazo alizisimamisha kwa muda kidogo.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako