Monday 24 March 2014

BEKHAM KUJENGA UWANJA WA KISASA WENYE CLUB NDANI KWA AJILI YA TIMU YAKE

Maajabu yanazidi kuendelezwa chini ya Jua na watu wenye umaarufu na pesa nyingi duniani wanaendelea kuonyesha jinsi wanavyoweza kutumia pesa za kufanya maajabu ya Dunia.
Hayo anadhamiria kuyafanya Mwanasoka Maarufu, David Bekham ambapo yupo kwenye mpango wa kujenga uwanja wa soka utakaokuwa ukitumiwa na timu mpya inayomilikiwa naye.
Picha za muundo wa Uwanja huo zimetoka ambapo utakua ni uwanja unaoweza kuingiza watu elfu ishirini na tano na unatarajiwa kujengwa katika eneo la Port of Miami, Marekani.
Unaambiwa pia ndani ya uwanja huu wa kisasa kutakuwa mgahawa mkubwa pamoja klabu ya usiku.
Kingine ni kwamba uwanja huu ambao bado haujapewa jina utakuwa ukichezewa mechi 17 kwa msimu wa ligi kuu ya Marekani. 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako