Sunday 2 February 2014

HAPPY BIRTHDAY TO MALIKA JOSEPH NGINILLA

Kwa Heshima ya pekee napenda kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kunijaalia siku ya leo (2/2/2014) kufikisha miaka kadhaa hapa duniani nikiwa bado nina afya tele.
Ninakumbukumbu nzuri kutoka kwa wazazi wangu waliniambia nilizaliwa Siku ya Alhamisi, saa Moja kasoro robo asubuhi katika Hospital ya Burhani katikati kabisa ya Jiji la Dar es Salaam.

Shukrani za Pekee ziwaendee wao maana malezi yao, Usimamizi wao na Msaada wao wa hali na mali, kunipenda kwao kwa dhati na kuwa na mimi bega kwa bega kumeweza kunifikisha hapa nilipo leo.

Siwezi kuwasahau Kaka na dada zangu wapendwa kwa kuwa na mimi kwenye shida na raha, tabu na magonjwa, siku zote nilizokuwa nao karibu hata nilipokuwa mbali walinijali na kunithamini kwa moyo mmoja, ni wengi kwa ujumla wao ila kwa kujali muda na nafasi wale woooote wenye majina ya ukoo yanayoishia na NGINILLA wanahusika sana.

Marafiki pia wanayo nafasi kubwa sana ya kunifikisha hapa nilipo, Kampani yao ya hali na mali, ushauri na kuhimizana kuyafikia malengo mbalimbali ya kimaisha kwa nguvu, uwezo na akili pia.
Wafanyakazi wenzangu wa maeneo mbalimbali,
Kuanzia Abood Media, DSJ, MSJ, GreenBelt College, Eden Hill College, Muslim University of Morogoro (MUM), Dar es Salaam Tv (DTV), Maisha Clubs zote CTN, Channel 10 na wote kwenye media mbalimbali mchango wenu sijafanikiwa kuusahau hata kidogo, nakumbuka na kuuheshimu sana.

Bila kusahau wale maadui zangu pia wamefanikisha uwepo wangu kwa njia moja ama nyingine maana bila wao kuweka vizingiti kwenye njia yangu ninayopita nisingeweza kutumia Uwezo wa akili na maarifa kuzikabili vizingiti hivyo hadi kufikia hapa, kiujumla wamenisaidia kuongeza uwezo wangu wa kufikiri na kutatua matatizo.
Wa mwisho japo sio kwa umuhimu ni mtu mmoja ambaye haitakuwa busara kumtaja ila ana mchango mkubwa sana katika maisha yangu na Siku kama ya leo imeweka maumivu sana moyoni mwake japo sio kwa makusudi ila MAPENZI YA MOLA NA YATIMIE
AHSANTENI SANA

By MALIKA JOSEPH NGINILLA - Chief Blogger @ PATAPICHA


No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako