Facebook wanazidi kujitanua zaidi
kibiashara katika ulimwengu huu wa dijiti ambapo wameweza kufanya makubalino na
waanzilishi wa ‘WhatsApp’, Jan Koum na Brian Acton kuinunua kwa makubaliano ya
jumla ya dola bilioni 19 pamoja na hisa.
Mwanzilisihi wa Facebook Mark
Zuckerberg amesema kuwa walianza kuzungumzia hatua hiyo siku 11 zilizopita ili
waweze kuimiliki WhatsApp ambayo hivi sasa inawatumiaji zaidi ya milioni 450
kwa mwezi.
Mwanzilishi wa WhatsApp ambaye alikuwa
mfanyakazi wa kampuni ya Yahoo!, Jan Koum ameonesha kulifurahia deal hilo na
kudai kuwa ni heshima kwao kwa kuwa mbali na pesa watakazolipwa, yeye pia
atakuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Facebook.
“We’re excited and honoured to patner
with Mark and Facebook as we continue to bring our product to more people
around the world.” Alisema Jan Koum.
Ingawa mmiliki wa Facebook anaamini
kwamba kwa kutumia WhatsApp wataweza kuwavuta mabilioni ya watumiaji,
amesisitiza kuwa hana mpango wa kuweka matangazo kwenye mfumo huo na kwamba
hadhani kama kuweka matangazo kwenye mfumo wa kutuma ujumbe ni njia bora zaidi
ya kutengeneza pesa.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo,
Facebook italipa fedha taslim dola bilioni 4 na kiasi cha hisa zake
kinachokadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 12, na ziada ya dola bilioni 3
zitakazolipwa baadae.
Deal hilo litakapokamilika na wakalipwa
kiasi hicho, waanzilishi wa WhatsApp Jan Koum na Brian Acton wanatarajiwa
kutangazwa kuwa mabilionea wapya.
Kampuni ya WhatsApp Inc. ilianzishwa
mwaka 2009 na watu wawili waliokuwa wafanyakazi wa kampuni ya Yahoo, mmarekani
Brian Acton na raia wa Ukrain Jan Koum, ambapo wanadai kuwa kwa hivi sasa
huwasajili watumiaji wapya milioni moja kwa siku.
Ikumbukwe ya kuwa mwaka May, 2009 Brian Acton alipeleka maombi ya kazi katika kampuni ya Facebook pamoja na
Twitter lakini maombi yake ya kazi yalikataliwa na hivyo akarudi mtaani na
kujipanga ambapo waliungana na Jan Koum kuanzisha WhatsApp.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako