Friday 21 February 2014

DIAMOND NA AY WAPATA SHAVU AFRIKA KUSINI


Siku chache kupitia mitandao ya kijamii mbalimbali kama Instagram,Facebook na Twitter, Diamond Platnumz amekua akipost picha nyingi akiwa nchiniAfrika kusini na wasanii mbalimbali wa Afrika akiwemo Dbanji.
Maswali yalikuwa mengi kichwani na mara nyingi tunaamini wasanii wanapokutana pengine wana mipango ya kushirikiana kwenye kazi za kisanii ama wana ukaribu mkubwa unaowafanya kuwa pamoja.

Blog hii imefuatilia na kugundua safari ya Diamond South Africa ni moja kati ya miradi ya One Campaign na hii ya sasa ni kupitia mradi wake wa Go Agric ambapo inahusu kufanya video na wimbo wa pamoja na zaidi ya wasanii 20 wa Afrika.

Video tayari imefanyika Johannesburg Afrika Kusini kwenye studio za M1 zinazomilikiwa na shirika la SABC, kwa Tanzania wasanii waliowakilisha ni AY na Diamond, wasanii wengine waliopo kwenye mradi huo ni pamoja na D’Banj, Femi Kuti wa Nigeria, Victoria Kimani wa Kenya na wengine.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako