Sunday, 5 January 2014

EUDOXIE AAHIDI KUFUNGA NDOA NA LUDACRIS JAPO AMEZAA NJE


Mpenzi wa muda mrefu wa Ludacris Eudoxie amefunga macho na kujifanya haoni ubaya alioutenda Ludacris kwa kupata mtoto nje ya uhusiano wao, ambapo ameahidi kufunga naye ndoa.
Habari kutoka rafiki wa karibu zinasema kuwa, Eudoxie ameshamsamehe Ludacris kwa kumpa ujauzito mama mtoto wa Luda, Tamika Fuller 
Luda alijitetea ya kuwa tulio hilo lilitokea bahati mbaya wakati wakiwa kwenye hatua za mwisho za kuachana na Tamika
Akimzungumzia Eudoxie, mpashaji habari amesema Luda yuko kwenye uhusiano na Eudoxie tangu 2009, na kiukweli imemuumiza sana kusikia taarifa hizo za mtoto, japo walipata nafasi za kuyaongea na kuyamaliza.

JUSTIN BEIBER - BADO NAMPENDA SERENA GOMEZ


Justin Beiber nbado inaonyesha anampenda mwanadada Selena Gomez baada ya kupost picha kwenye mtandao akiwa amekumbatiana na mwanadada huyo 
Katika picha hiyo Beiber ameweka saini yake na kuandika maneno yafuatayo "Love the way you Look at me" akimaanisha anampenda jinsi anavyomuangalia.
Mikono ya mwanadada Serena inaonekana imemkumbatia beiber akimuangalia kimahaba.
Post ya mwisho ambayo Serena Gomez aliyoitoa mapema wiki hii kuhusiana na Justin Beiber (JB) ni kuwa "Every woman learns -- you can't resist the Biebs" 

MUDADA AJIFUNGUA MAPACHA WANNE KWA MPIGO


Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, amejifungua watoto wanne mapacha kwa mkupuo (Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya. 
Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi.
Watoto hao mapacha wana uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi na wapo katika hali nzuri 

LIONEL MESSI AKIWA TANZANIA KWENYE MLIMA KILIMANJARO

 

MENEJA WA SCHUMACHER AWASHUTUMU MADAKTARI


Meneja wa bingwa zamani wa mashindano ya Formula One, Michael Schumacher amewashutumu baadhi ya madaktari wanamtibu mteja wake kwa kile alichokiita ripoti isiyo ya kweli juu ya afya ya dereva huyo.
Schumacher aliripotiwa kuwa kwenye hali mbaya huku maisha yake yakiwa hatarini baada ya kuumia vibaya kwenye ajali iliyotokea kwenye milima ya ufaransa alikokuwa akishiriki mchezo wa kuteleza kwenye barafu .
Meneja huyo amesema kuwa pamoja na hali ya Schumacher kuwa mbaya lakini haijafikia hatua ya maisha yake kuwa hatarini na anaendelea na matibabu katika hospitali aliyofikishwa

Saturday, 4 January 2014

MSANII DAYNA NYANGE ATOA YA MOYONI JUU YA WATU WALIVYOPOKEA TAARIFA YA KUSHIKWA KWA VIDEO QUEEN JACK CLIFF

MSANII WA KIZAZI KIPYA DAYNA NYANGE
Jamani hivi ni nani kwenye Mgongo huu wa dunia ambaye hajawai kukosea?!
Wapo binadamu wenzetu wanamakosa makubwa na hatuyajui na mengine yanajulikana....
Kwanini tumekuwa mstari wa mbele kuwanyooshea watu vidole pale wanapokosea tena na kuwaombea Mabaya....... Dah!
Tukumbuke Sisi sote ni binadamu akuna anaejua kesho yake
Sina maana tutetee uovu au kosa linapofanyika bali tutumie muda kutafakari kabla ya kumhukumu MTU..
Wanawake wenzangu huyu ni Mwanamke mwenzetu lakini sisi ndio tumekuwa mstari wa mbele kumlaani Na kutolea maneno machafu Na hali Yakuwa tunajua hakuna alie mkamilifu
Binafsi imeniuma Na nimejiskia vibaya sana

SAWA KAFANYA KOSA
Ila tusiwe majaji wa kutoa hukumu anza kujihukumu kwa maovu yako kabla ya kumuhukumu mwenzako
Tafakari maovu yako kabla kumnyooshea kidole mwenzako

Tuache mamlaka za sheria zifanye kazi yake
Wanawake wenzangu TUPENDANE Na tuwe na umoja Tushirikiane na tushauriane katika maamuzi yetu madogo Na makubwa labda tutaepuka ili tatizo
Inawezekana haya yote yanatokea kwetu sisi kwa kukosa ushirikiano Na upendo

JACK DADA ANGU UMEKOSEA
Ila Sina sababu ya kukulaumu au kukuhukumu
wakati mwingine binaadamu ujifunza katokana Na makosa Mungu ni wetu sote Inshaallah atakusimamia katika hili.
Nimeshidwa kuvumilia nimeamua kusema nilichosema ila kama Kuna nilie mkwaza
naomba Aniwie radhi.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU TUBARIKI WATANZANIA
By Dayna nyange

LUDACRISS AMSALITI MCHUMBA WAKE NA KUZAA NJE


Licha ya kuwa kwenye uhusiano ya muda mrefu na mchumba wake Eudoxie, Ludacris bado ametoka nje ya uhusiano wao.
Hivi karibuni habari zimetoka kwamba Ludacris amepata mtoto nje ya uhusiano wake kitu ambacho kinatafsiliwa kwamba alitoka nje ya uhusiano wake.
Mama wa mtoto huyo amejulikana kwa jina la Tameka Fuller ambaye alisoma pamoja na Ludacris kupindi cha high school na walikuwa na uhusiano kipindi hicho.
Ludacris ana mtoto mwingine wa kike na hivi sasa amepata binti mwingine anaitwa Cai Bella Bridges na bado anaendelea kuwa na uhisiano na Eudoxie.
Ludacris hajakataa kuwa baba wa mtoto huyo japokuwa ripoti zinasema kwamba ametaja kiasi kidogo sana cha pesa ambacho atatoa kwa ajili ya malezi ya mwanae(child support) ukilinganisha na kipato chake anachopata

BI. KHADIJA KOPA AKANUSHA KUWA NA ACCOUNT YA FACEBOOK


Malkia wa Mipasho bi. Khadija Kopa akanusha kuwa na account ya facebook na badala yake ametahadharisha washabiki wake kuwa, kuna utapeli ambao unaendelea na kuna mtu anatumia jina lake
Amewataka mashabiki wake wasidanganyike na utapeli huo na tayari keshatoa taarifa polisi.
 

UJIO MPYA WA SNURA MWAKA 2014


Miongoni mwa wasanii wa Bongo fleva ambao hawatoweza kuusahau mwaka 2013 pengine Snura nae yupo kwenye list na hii ni baada ya meneja anayesimamia kazi zake za muziki Hemed Kavu au HK kuzungumzia mafanikio yote ya mwaka 2013 aliyoyapata staa huyu wa ‘Majanga
Hk anaanza kwa kusema "Kiukweli mwaka 2013 tulifanya vitu vingi vikubwa kwa sababu naamini msanii wangu ni msanii pekee wa kike aliyefanya show nyingi hata kwa wanaume hakuna anayemfikia Snura kuna show tunafanya hadi J’4, J’5 hadi alhamisi tumekua tukizifanya show hizo.
‘Kwa ujumla kuhusu pesa tulizoingiza kwa mwaka 2013 ni mpunga mrefu kwa sababu tumefanya show zisizopungua 180 kwa mfano tunapiga Njombe, tunapiga Songea, tunapiga na Mbinga so kwa wiki tuna uhakika kwa wiki tunafanya show zisizopungua 4 hadi 5
‘Ngoma ya Majanga ime-hit mwez wa 3 ndo tukaanza kukamata show lakini kabla ya hapo tulikua na nyimbo ya shogaake mama na debe la vanga na tulikua tunafanya show pia, tuna jumla ya show kama 20 za makampuni na hizi ni zile tunalipwa milion 3 hadi milion 4.
‘Kwa siku tunaweza kupiga show hadi 3 kwa mfano kuna siku tulikua na show Z’bar tukaja Dar kulikua na show ya kampuni pale Amana, tukatoka hapo tukawa na show mchana huo huo na usiku tukapiga tena show, Mpunga ni mrefu ni zaidi ya Milion 100′.
‘Kuna dili tulikua tumepata ya Snura kuwa balozi wa kampuni fulani lakini mkataba ndo tunaweza kusaini mwezi huu ambao utakua ukihusisha pia na show kwa Snura ambapo watatoa shows 30 ambazo kila show moja tutakua tukifanya kwa milioni 7 kwa hiyo kuna Milion 210 zipo’.
‘Kwa Snura mwaka 2014 amekuja na mavazi yake ambayo tumebuni wenyewe kwa hiyo kuna style mpya ya mavazi na moja kati ya wasanii wanaovaa nguo za heshima ni pamoja na Snura japo mwili wake ndo una tetemesha lakini ndo kaumbwa hivyo inabidi tukubali’Hk

Wednesday, 1 January 2014

MARIAH CAREY ATUPIA PICHA ZAKE ZA KWANZA KWA MWAKA 2014

Mariah Carey ametupia picha hii Dakika 58 zilizopita (saa 8:12am - za Kitanzania) na kutupia maneno yafuatayo "Happy new year!!!"
 
Mariah Carey ametupia picha hii Saa 2 zilizopita (Saa za Hapa kwetu ilikuwa saa 12:14 asubuhi) kutupia maneno yafuatayo "Happy New Year!!!! "You like this and you know it"!!!

MWANAHIP-HOP WA MAREKANI AANDIKA POST YENYE NENO LA KISWAHILI

 
Mwaka mpya wa 2014 tunauanza vizuri kabisa watanzania baada ya siku moja kabla ya kuumaliza mwaka huo wa 2013 msanii wa Marekani wa mtindo wa kufoka foka ameandika status kyenye neno la Kiswahili kwenye Account yake.
Talib Kweli (38), aliweka neno la Kiswahili kwenye moja ya sentensi zake ndani ya mtandao wa twitter alio na wafuasi zaidi ya laki nane huku akiwa anafwatwa na mastaa kadhaa wa bongo akiwemo Nikki wa II, Godzilla, Profesa Jay, Chidi Benz, Fid Q, Vanessa Mdee na wengine.
Wakati kilipotokea kifo cha mzee Nelson Mandela, staa wa hiphop duniani Nicki Minaj alimiliki headlines kwenye nchi zinazoongea Kiswahili baada ya kuandika ujumbe kuhusu mzee Mandela na kisha kumalizia kwa kuandika kiswahili ‘madaraka kwa wote’ kwenye page yake ya Instagram.

DIAMOND ALIVYOFUNGA MWAKA NDANI YA LINDI

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya anayetikisa Nchi ya Tanzania na Africa kwa Ujumla, Naseeb Abdul almaarufu kama Diamond, ameuanza mwaka mpya na wananchi wa Lindi katika tamasha la kudumisha Amani na maendeleo lililodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mhe. Bernard Membe.
Tamasha hilo limefanyika usiku wa kuamkia mwaka 2014 katika uwanja wa Ilulu Manispaa ya Lindi ambapo Diamond amezikonga vyema vyoyo za wananchi wa Mkoa huo.
 
Mbunge aliyemwalika Diamond ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe, Bernard Membe naye alikuwepo sambamba na wananchi wa Lindi kushuhudia shoo hiyo iliyoambatana na kuukaribisha mwaka 2014

UTARATIBU WA BAR MWAKA 2014


UJUMBE ALIOANZA NAO MWAKA 2014, JOYCE KIRIA KWA WAKINADADA


Hakianan huu ujumbe nauleta kwako kwa nia njema kabisa kwa ajili ya kumaliza 2013.
we Mwanamke mwenzangu ambae mpaka sasa bado unategemea mwanaume akuendeshee maisha kwa kila kitu, hakika unaitaji Ukombozi..
Siyo dhambi kama ukipata mwanaume anaekugaramia kwa vitu mbalimbali kwa hiari yake na mapenzi yake..siyo kwa kudai kama vile umemwajiri au ulimkopesha!!
Tatizo letu wengine tunawalazimisha wapenzi wetu watufanyie vitu kwa nguvu na asipofanya hivyo Utanunaje sasa!! 
Mbaya zaidi Mara nyingi mnaomba vitu ambavyo wapenzi wenu hawana uwezo navyo! Na wewe mwenyewe mwanamke umeshindwa kujiuliza kwamba mbona wewe huna hivyo vitu unavyolazimisha ununuliwe? Yeye akaibe??
Unakuta mtu katongozwa tu! Anaanza oooh kodi imeisha, oooh nadaiwa ada, nataka galax note3, oooh nataka kiwanja, oooh nataka nyumba, oooh nataka gari, vocha, bili ya maji, umeme, nauli ya kwenda kusalimia ndugu na jamaa, oooh simu ya mama, !! Kiruuuuuuuu ndo maana wanaume wenye akili zao wanatoka baru...
Jamani wanaume siyo Migodi! Nao wanatafuta pesa kwa tabu sana.siku hizi maisha ni magumu sana, Ujumbe wangu wa kuanza 2014 Tushirikiane kuleta maendeleo yetu pamoja badala ya kugeuzana ATM...
Huu ujumbe kama umekugusa hakikisha unaingia 2014 ukiwa na mtazamo mpya tofauti na huo wa Kitumwa na epuka kabisa kuwa Mzigo kwa mwenzako....kuwa msaada kwake ili maisha yawe mepesi...
Hata wanaume siku hizi wapo Magolikipa...acheni siyo fresh

Mbutaaaaaa...

NOTE: USISAHAU OPERESHENI TOKOMEZA MICHANGO YA HARUSI NA SHEREHE 2014..Tuchangie maendeleo..

TV KUBWA ZAIDI YA KITANDA YAINGIA SOKONI


KAMPUNI YA KIKOREA SAMSUNG IMEINGIZA SOKONI TV MPYA YENYE UPANA WA INCH 102 NA UREFU WA INCHI 70,UKUBWA AMBAO NI ZAIDI YA KITANDA KIKUBWA.
KWA MARA YA KWANZA KOREA KUSINI IKIWA INAUZWA 160MILLION WON YA KOREA KUSINI NI SAWA NA SHILINGI MILIONI 241 ZA KITANZANIA
TV HII INATUMIA TEKNOLOJIA YA U-HDTV(Ultra-High Definition Television) INAYOSABABISHA PICHA KUONEKANA VIZURI ZAIDI YA MARA NNE YA TV ZA HD ZA KAWAIDA
IMEANZA KUUZWA JANA (30DEC) KOREA KUSINI,LAKINI BAADAE ITAANZA KUUZWA AU KUPATIKANA SEHEMU MBALIMBALI ZA DUNIA!!

STATUS YA MWISHO YA LADY JAYDE KATIKA MWAKA 2013


KWA WALE WAJANJA WA MJINI WATAPAJUA HAPA

 

PICHA YA KUANZIA MWAKA 2014