Wednesday 4 February 2015

MATOKEO MECHI YA FA MAN UNITED VS CAMBRIGDE UNITED


Na huko Barani ULAYA
KLABU ya Manchester United imetinga Raundi ya Tano ya Kombe la FA baada ya ushindi wa mabao 3-0 Cambridge United Uwanja wa Old Trafford.

Timu ya kocha Mholanzi Louis Van Gaal iliyolazimishwa sare katika mchezo wa kwanza na wapinzani wao hao ugenini, jana ilikuwa tofauti katika mchezo wa pili wa Raundi ya Nne.

Juan Mata alianza kuwafungia bao la kwanza Mashetani Wekundu dakika ya 25, kabla ya Marcos Rojo kufunga la pili dakika ya 32 na James Wilson kumalizia la tatu mnamo dakika ya 73.

Sasa, Man United itasafiri kuwafuata Preston North End katika Raundi ya Tano Jumatatu ya Februari 16, mwaka huu.

Kikosi cha Man Utd jana kilikuwa: De Gea, McNair, Smalling, Evans, Rojo/Young dk81, Blind, Rooney, Di Maria/Herrera dk71, Mata, Van Persie/Wilson dk66 na Fellaini. 

Cambridge Utd: Dunn, Tait, Nelson/Miller dk87, Coulson, Greg Taylor, Donaldson, McGeehan, Champion, Chadwick/Morrissey dk51, Elliott na Simpson/KaiKai dk61. 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako