Katika Jiji la Madrid huko uhispania kulikuwa
hapatoshi katika mchezo uliowakutanisha Miamba ya jiji hilo, Atletico Madrid na
Real Madrid ambazo zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 0-0 katika
mchezo wa kwanza wa Kombe la Mabingwa barani Ulaya, hatua ya robo fainali.
Atletico waliowakaribisha Real katika mchezo
uliochezwa katika dimba la Vicente Calderon, ambapo timu hizo zitarudiana
katika uwanja wa Santiago Bernabeu tarehe 22 Aprili.
mlinda mlango wa Atletico Madrid Jan Oblak
alikuwa kikwazo kwa real, ambaye alinga'ara katika mchezo huo kwa kupangua
michomo mikali kadhaa ya wachezaji wa Real Madrid walokuwa wakilisakama lango
la atletico, huku Mario Suarez wa Atletico Madrid akikosa nafasi ya kuifungia
timu yake mwishoni mwa mchezo huo.
Naye winga Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth
Bale aliyekosa nafasi muhimu mapema katika dakika ya tatu ya kipindi cha kwanza
cha mchezo kwa kushindwa kutumbukiza mpira wavuni amesema walistahili kushinda,
ingawa haikuwa hivyo.
“NI MATOKEO MAZURI KUENDEA HATUA YA MARUDIANO
KWA SABABU HATUKURUHUSU GOLI LOLOTE. KWA UPANDE WANGU NAFKIRI TULITAKIWA
TUSHINDE, TULISTAHILI KUSHINDA KWA SABABU KIPINDI CHA KWANZA TULICHEZA VIZURI
ZAIDI YA ATLETICO BAHATI MBAYA HATUKUWEZA KUENDELEZA KIWANGO KILE KILE KIPINDI
CHA PILI”.
Katika mchezo huo Mlinda mlango wa Real Madrid
na timu ya taifa ya Hispania Iker Casillas ameweka historia yake kwa kuwa
mchezaji aliyecheza michezo mingi zaidi katika michuano hiyo kwa kufikisha
michezo 147 akimzidi mchezaji wa Barcelona xavi Hernandez.
Mechi hii jana pia imeweka rekodi kwa Vijana
wa Carlo Ancelotti kuwa ni mchezo wao wa saba kukutana na Atletico Madrid bila
kushinda.
Mchezo mwingine
uliochezwa jana usiku ulizikutanisha timu Juventus ya Italia na Monaco ya Ufaransa,
Matokeo ya mchezo huo Juventus iliibuka na ushindi wa goli 1-0. Juventus
ilipata bao lake pekee katika dakika ya 57 kwa njia ya penalti ikifungwa na
Arturo Vidal.
Hata hivyo kocha wa Monaco Leonardo Jardim,
ameilalamikia penalti hiyo kuwa haikuwa ya haki. Timu hizi nazo zitarudiana
huko Monaco April 22.
Juventus inalenga pia kufika hatua ya nusu
fainali ambapo kwa mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2003.
Wakati huo huo, winger wa monaco Nabil Dirar
anaamini mshambuliaji wa timu hiyo aliye kwa mkopo katika timu ya man utd
Radamel Falcao atafkiria kurudi Monaco na anatamani asingeondoka Monaco.
Falcao alitimkia man utd kwa mkopo wa muda
mrefu lakini amekuwa katika wakati mgumu chini ya van gaal ambaye amekuwa
akimuweka benchi.
Mshambuliaji huyo raia wa Colombia amefunga
goli nne tu kwa man utd hali inayopelekea utd kusita kulipa kiasi cha pauni
milioni 53 ili kumsajili kwa ujumla.
Michezo mingine miwili ngazi ya robo fainali
itaendelea leo usiku ikizikutanisha timu ya FC Porto ya Ureno dhidi ya Bayern Munich
ya Ujerumani, huku Paris Saint Germain ya Ufaransa ikiikaribisha Barcelona ya
Hispania.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa aina kutokana
na kila timu kuonekana kuwa tishio kwa wapinzani wao.
Timu ya PSG itakosa huduma ya mshambuliaji
wake hatari Zlatan Ibrahimovic ambaye anatumikia adhabu ya kadi nyekundu
aliyopewa dhidi ya mechi na Chelsea pamoja na Aurier, kwa upande wa majeruhi
watakosa huduma ya Thiago motta pamoja na mlinzi wao david luiz aliye na hati
hati ya kucheza.
Kwa upande wa barca wataikosa huduma ya Dani
alves pamoja na Thomas vermaelen.
Hata hivyo kocha wa PSG Laurent Blanc amesema
hadhani kama falsafa za Barcelona zimebadilika sana na kuongeza kuwa ni kweli
wanamiliki mpira vizuri na wana nguvu ingawa na wao wanapenda kumiliki mpira.
Blanc amesema wanaweza kuwafunga barca kwani
wao ni moja ya timu chache zilizowahi kuwafunga Barca goli 3.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako