Raisi Pierre Nkurunzinza |
Tukiangazia hali ya
mambo nchini Burundi aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare
ametangaza Jumatano hii kuwa rais wa
nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani.
Hayo yanajiri wakati Rais Pierre
Nkurunziza anashiriki mkutano wa kikanda wa marais wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki kuhusu mgogoro unaoendelea nchini Burundi.
Burundi imekua ikishuhudia
maandamano ya raia wakipinga muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza. Kwa muda wa
majuma kadhaa mitandao ya kijamii, na vyombo mbali mbali vya habari vimekuwa
vikiripoti taarifa hizo kutoka huko Burundi
Mpaka sasa
haijajulikana kundi gani lina mamlaka ya uongozi wa nchi, baada ya kundi la
wanajeshi linaloongozwa na jenerali Godefroid Niyombare kutangaza kuipindua
serikali ya Pierre Nkurunziza.
Hata hivyo Ikulu ya rais huyo imeendelea
kutangaza kupitia akaunti yake ya twitter kuwa mapinduzi hayo yamefeli, baada
ya jeshi kuingilia kati na kudhibiti hali ya mambo.
Kituo cha habari cha Burundi RTBN kimemhoji rais Pierre
Nkurunziza kwa simu mwendo wa saa sita.Vita vimezuka karibu na afisi za kituo
hicho cha habari.Jenerali anayeunga mkono jaribio hilo la mapinduzi amekiambia
chombo cha habari cha AFP kwamba vitengo vinavyopigana kumpindua vimepata agizo
la kukiteka kituo hicho habari cha RTNB kwa kuwa wana uwezo.
Mgogoro wa Burundi umezusha wasi wasi wa kurejea katika ghasia
baada ya miaka kumi na miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Zaidi ya watu elfu tatu walikufa katika vita vya kikabila kati
ya wahutu na watutsi; vita vilivyomalizwa muongo uliopita.na mgogoro wa sasa
nchini humo umehusisha kwa kiasi kikubwa na masuala ya kisiasa.
lakini,yaliyojiri Burundi hayana tofauti na kilichojiri katika nchi jirani ya
Rwanda ambayo ilikumbwa na mauaji ya kimbari nayo ilikabiliwa na masuala ya
ukabila.
Rais Piere Nkurunzinza alizaliwa desemba 18/1963 mjini Bujumbura
katika familia ya wahutu
Na baba yake Yustach Ngabisha alikuwa mbunge wa Burundi mwaka
1965 aliuwawa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwaka1972
Jenerali Godefroid Niyombare |
Meja Jenerali Niyombare ambae ndie ametangaza mapinduzi hayo
nchini Burundi, aliteuliwa kuwa kamanda mkuu wa jeshi la Burundi mwaka
2014 akichukua nafasi ya Adolphe
Nshimirimana akiwa anatokea nchini Kenya kama balozi wa Burundi
Lakini alitumuliwa na Nkurunzinza kama mkuu wa usalama February
2015 bila kutolewa sababu za uamuzi huo
Umoja wa mataifa umeonya hivi karibuni kwamba ikiwa ghasia
zitasitishwa Burundi itakuwa na Amani na kama itakuwa vinginevyo basi nchi hiyo
itarejea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe .
watu zaidi ya 20 wameuawa tangu tarehe 25 mwezi
uliopita baada ya Nkurunzinza kutangaza kuwania muhula wa tatu madarakani
kinyume na katiba ya taifa hilo ambayo inaruhusu mihula miwili tu ya miaka
mitano kila mmoja akidai muhula wake wa kwanza alichaguliwa na bunge na wala
sio wananchi. Zaidi ya waburundi 50,000 wametorokea nchi jirani kufuatia ghasia
za kabla ya uchaguzi wa mwaka huu
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limeitisha kikao
cha dharura kujadili hali ya mambo Burundi baada ya jenerali mwandamizi jeshini
kutangaza kunyakua madaraka kutoka kwa Rais Pierre Nkurunziza. Kikao hicho cha
dharura kimeitishwa na Ufaransa huku katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki-moon akitoa wito wa utulivu na ustahamilivu nchini Burundi. Wakati huo huo
Umoja wa Mataifa unafuatilia kwa karibu kinachoendelea nchini Burundi na
kusisitiza kauli ya Katibu Mkuu Ban Ki-moon aliyotoa wakati wa mkutano wa
viongozi wa umoja wa Afrika huko Addis Ababa, Ethiopia kuhusu awamu za uongozi.
Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane
Dujarric aliyezungumza mjini New York, wakati wa mkutano na waandishi wa habari
waliotaka kufahamu msimamo wa chombo hicho kuhusu hali iliyoripotiwa nchini Burundi.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako