NAIBU WAZIRI WA HABARI JULIANA SHONZA KUSHOTO AKIPATA MAELEKEZO KUTOKA KWA VIONGOZI WA TBC |
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Juliana Shonza amewaasa wanahabari kutumia vizuri taaluma yao
katika kutoa habari zenye weledi zinazoleta manufaa kwenye jamii na kusisitiza
kuwa endapo taaluma hiyo ikitumika vibaya inaweza kusababisha madhara makubwa
sana kwa jamii.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika
makao makuu ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) barabara ya TAZARA jijini
Dar es Salaam, Naibu Waziri Shonza amesisitiza ushirikiano kati ya serikali na
wanahabari ili kuipeleka mbele zaidi taaluma ya habari nchini.
Vile vile Naibu Waziri Shonza
ameipongeza TBC kwa kuwaamini vijana na kuwapa fursa kubwa ya kufanya kazi na
kuendana bega kwa bega na sera ya serikali inayosisitiza kutoa nafasi nyingi
kwa vijana katika kulitumikia taifa.
Amesema anashukuru sana kwa ushirikiano
aliopewa na TBC na kusisitiza kuwa kwa kushirikiana na Waziri Mwenye dhamana ya
wizara hiyo wanashughulikia changamoto zote zinazolikabili shirika hilo.
Ameipongeza TBC kwa kuwa mfano bora
miongoni mwa vyombo vingi vya habari nchini na kuviasa vyombo vingine kufuata
misingi bora ya taaluma ya habari.
NAIBU WAZIRI AKIWA NDANI YA STUDIO ZA TBC INTERNATIONAL |
Hii ni ziara ya kwanza kwa Naibu Waziri
Shonza kufika TBC tangu alipoteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli Oktoba saba
mwaka huu akichukua nafasi ya Anastazia Wambura.
NAIBU WAZIRI SHONZA ALIPOTEMBELEA STUDIO ZA TBC FM |
Habari/picha
Hamisi Hollela na Mahmud Rajab
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako