Monday, 15 August 2016

MECHI ZA EPL WEEKEND HII

LIVERPOOL PLAYER COUTINHO
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema ushangiliaji wake pamoja na wachezaji wa Liverpool baada ya ushindi dhidi ya arsenal hauruhusiwi.
Katika mchezo wa ligi kuu ya england uliochezwa jioni ya jana jijini London, wenyeji wa emirates arsenal waliangukia pua baada ya kupata kipigo cha magoli 4-3 kutoka kwa majogoo wa anfield Liverpool.
Liverpool iliyochini ya klopp imeanza kampeni ya kusaka ubingwa wa epl kwa ushindi mnono licha ya arsenal kutangulia kufunga katika kipindi kwanza kupitia kwa goli lililofungwa na theo Walcott katika dakika ya 31 lakini kabla kipenga cha mwamuzi kupulizwa kuashiria kipindi cha kwanza kumalizika philipe coutinho aliisawazishia Liverpool kupitia mkwaju wa mpira wa adhabu ulizama wavuni katika dakika ya 45.
Katika kipindi cha pili Liverpool waliongeza idadi ya magoli dhidi ya wapinzani wao ambapo katika dakika ya 49 adam lallana aliukwamisha mpira wavuni kabla ya coutinho kurejea tena wavuni katika dakika ya 56 na saido mane kushindilia msumari wan ne katika dakika ya 63.
Arsenal walikusanya nguvu na dakika moja baada ya goli la mane, alex oxlade chamberlane aliifungia arsenal goli safi akiivuruga safu ya ushambuliaji ya Liverpool na calum chambers akifunga la tatu katika dakika ya 75.
 “sikupaswa kushangilia goli la nne wakati ilibaki nusu saa nzima. Nilifahamu kwa wakati ule lakini nilishachelewa”.
Aidha klopp amesema kilichomfurahisha zaidi katika ushindi huo ni namna ambavyo walitulia na kujilinda katika kipindi cha dakika 30 za mwisho ambapo arsenal walizidisha mashambulizi na hata kupelekea kuonekana huenda isingekuwa siku yao kushinda.
Upande wa pili wa shilingi mambo si shwari kwa kocha wa arsenal arsene wenger ambaye kikosi  chake kinazidi kuandamwa na majeruhi. Pamoja na kipigo cha ufunguzi asrenal imepata pigo la majeruhi baada ya mshambuliaji kinda wa timu hiyo alex iwobi kupata majeraha sambamba na kiungo aaron ramsey ambao walilazimika kutolewa nje kabla ya mechi kumalizika.
Kwa upande wake Kocha wa Manchester united Jose Mourinho ameelezea kufurahishwa na kiwango alichokionyesha kiungo Juan mata baada ya kufunga goli katika mchezo wao dhidi ya Bournemouth.
Mata alifungua ukurasa wa magoli wa united msimu huu baada ya kupachika goli dakika 5 kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika na kuipa uongozi united katika dimba la vitality, kabla ya wayne rooney na Zlatan Ibrahimovic kuongea mengine mawili katika kipindi cha pili.
Adam Smith aliifungia Bournemouth goli la pekee lakini kikosi hicho cha mourinho kilipigana kuwazuia Bournemouth kuongeza mengine mpaka mpira kumalizika na kujinyakulia pointi tatu muhimu.
Mata ambaye aliuzwa united na mourinho alipokuwa Chelsea alifanyiwa mabadiliko ya kutolewa nje baada ya kuingia uwanjani katika mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Leicester na sakata hilo kuleta mtazamo tofauti baina ya mashabiki wa united lakini mourinho ni kama aliwajibu mashabiki hao kwamba hakuna kitu yao na kuamua kumuanzisha mata katika mchezo wa jana na mourinho kusema ilikuwa mechi sahihi kwa mata kuonyesha kiwango chake.
“lilikuwa goli muhimu lenye kutumia akili, goli kutoka kwa mtu wa mpira. Namjua vizuri kwasababu nimefanya nae kazi kwa miezi sita tulipokuwa Chelsea, najua fika kipi anachoweza kutoa na kipi asichoweza”.
 Mourinho ameongeza kuwa anafuraha kwa mata lakini pia anafuraha kwa timu nzima hata wale waliokuwa nje na kuingia kutoa mchango wao katika ushindi na hata wasiopata nafasi ya kucheza kwani wote kwa pamoja wanajenga familia moja.
Mechi inayofuata united watawakaribisha Southampton old Trafford na mourinho kuwa na mtazamo chanya kuelekea mchezo huo hasa baada ya kupata ushindi mfululizo.
@@@@@@@@@@@@@
Nae kocha wa Manchester city, pep guardiola amekiri kwa mlinda mlango wake joe hart kuchukizwa kwa kuachwa katika kikosi cha man city wakati timu hiyo ikianza mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi wa ligi kuu ya epl.
Mara baada ya kuteuliwa kuwa kocha mpya wa timu hiyo, guardiola hakuchelewa kubadilisha baadhi ya vitu ikiwa ni sambamba na kumuacha mlinda mlango huyo ambaye si tu chaguo la kwanza kwa klabu ya man city lakini pia ni mlinda mlango nambari moja wa timu ya taifa ya England.
Hart aliishuhudia timu yake siku ya jumamosi ikishinda magoli 2-1 dhidi ya sunderland akiwa nje na kitendo hicho kuibua tetesi za mlinda mlango huyo kutimka city.
Guardiola amesema ana uhakika kwamba hart amechukia, lakini si kila mchezaji asiyepata nafasi katika kikosi kitakachoanza atauzwa bali amesema kuwa anatakiwa achague timu na kwa sasa ana wachezaji 28 na kati ya hao wanatakiwa wamshawishi zaidi uwanjani.
Licha ya kuwa na msimu mzuri 2015/2016 na kuwa mchezaji muhimu wa man city katika miaka ya hivi karibuni lakini kushindwa kuonyesha makali katika michuano ya kimataifa ya euro mwaka kumeifanya klabu ya man city kuhusishwa na kutaka kusajili magolikipa wengine huku taarifa hizo zikichagizwa zaidi na ujio wa pep guardiola.
Hata hivyo guardiola ametupilia mbali taarifa za kumshusha hart na kusema bado mlinda mlango huyo anaweza kuwa chaguo lake la kwanza na kutetea uamuzi wake wa kumuanzisha langoni willy caballero kwani muarjentina huyo alianza mazoezi mapema kabla ya joe hart.

@@@@@@@@@@@@@@@

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako