Friday 7 April 2017

WASANII ROMA , MONI KUTOKA CENTRAL ZONE NA WATU WENGINE WAWILI WATOWEKA

Wasanii wawili kutoka Tanzania Ibrahim Mussa ajulikanae kama Roma Mkatoliki na Moni pamoja na producer wa Togwe records Bin laden na Emma ambaye ni mfanyakazi wa mama mzazi wa mmiliki wa studio za tongwe records J Murder wametoweka katika mazingira ya kutatanisha wakiwa katika studio hizo za togwe baada ya kuvamiwa na kuchukuliwa na watu wasiojulikana katika gari aina ya noah;J murder ameeleza kushtushwa na tukio hilo na kuongeza kua watu hao walibeba baadhi ya vifaa vya studio na kuondoka navyo.
Baada ya tukio hilo mmiliki wa tongwe rec J Murder alifika kituo cha polisi cha Oysterbay na kuripoti juu ya tukio hilo.

Nae Nancy mke wake roma anaeleza kua simu ya mume wake inaita tu bila kupokelewa na hadi hivi sasa hajui mume wake yupo wapi.
Wasanii kwa umoja wao wameungana kuweza kufatilia swala hilo ambalo hadi hivi sasa hakuna anaejua wasanii hao wako wapi.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako