Friday 14 April 2017

MBADALA WA BABU WENGER

London, England .Arsenal imeanzisha mazungumzo na kocha wa Juventus, Max Allegri wakati hatima ya Arsene Wenger ikiwa njia panda.
Gazeti la SunSport limebainisha kuwa Gunners imekuwa na mawasiliano na Allegri katika siku saba zilizopita katika kuangalia uwezekano wa kumchukua Mtaliano huyo kushika mikoba ya Wenger.
Hivi karibuni kiongozi moja wa Arsenal alikuwa hafahamu kama Wenger ataendelea kubaki klabu hapo, wakati kocha huyo akiendelea kupata matokeo mabovu na kuongeza shindikizo kutoka kwa mashabiki.
Pia, kuna taarifa kuwa klabu hiyo inahitaji mkurugenzi wa ufundi na winga wa zamani wa klabu hiyo Marc Overmars ametajwa kujaza nafasi hiyo.
Hata hivyo, Wenger anajua kuwa kuna mambo yanayoendelea nyuma yake.
Mwenendo wa kusuasua wa Arsenal kwa sasa umewalazimisha viongozi kumfuatilia Allegri ( 49) mwenye mafanikio makubwa kwa sasa.
Mtaliano huyo ametwaa ubingwa wa Serie A na Kombe la Italia katika misimu yake miwili ya kwanza akiwa na Juventus na sasa pia yuko katika nafasi nzuri ya kutwaa taji msimu huu.
Jumanne iliyopita aliingoza Juventus kuichakaza Barcelona kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Jambo zuri zaidi ni kwamba Allegri mwaka jana alimaliza masomo yake ya Kiingereza akiwa ni maandalizi ya kuachana na miamba ya  Serie A na kutimukia Ligi Kuu England.
Kocha huyo pia alikuwa akitakiwa na Chelsea kuziba pengo la Jose Mourinho, lakini kwa bahati mbaya nafasi ikaangukia kwa  Antonio Conte

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako