Friday, 6 February 2015

UWANJA WA MALABO WAGEUKA VITA BAADA YA WENYEJI GUINEA KUPIGWA 3 BILA NA BLACK STARS



NDOTO za wenyeji Equatorial Guinea kunyakua Kombe la Mataifa ya Afrika zimeyeyuka usiku wa jana baada ya kufungwa mabao 3-0 na Ghana Uwanja wa Malabo.

Black Stars inayofundishwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Avram Grant ilipata mabao yake kupitia kwa Jordan Ayew kwa penalti dakika ya 42, Mubarak Wakaso dakika ya 45+1 na Andre Ayew dakika ya 75.

Baada ya bao la tatu, huku Ghana wakiendelea kuwashambulia wenyeji, zikiwa zimesalia dakika nane mchezo kumalizika, mashabiki wa Guinea walianza kurusha chupa uwanjani na pia kuwapiga nazo mashabiki wa Ghana, ambao walilazimika kuvamia uwanjani kunusuru maisha yao.

Polisi walilazimika kutumia hadi helikopta kuwaondoa uwanjani mashabiki wa Guinea na baada ya nusu saa hali ilipotulia Uwanja ulikuwa kama mtupu na refa Eric Castane akamalizia mchezo.  

Ghana sasa itamenyana na Ivory Coast katika fainali ya AFCON 2015 Jumapili, wakati hatma ya wenyeji na mchezo wa mshindi wa tatu dhidi ya DRC haijajulikana, kwani kuna uwezekano wakapewa adhabu kali na CAF. 

Thursday, 5 February 2015

GERRARD ACHEZA MECHI YA MIA 7 WAKATI LIVERPOOL WAKIIUA BOLTON 2 - 1



LIVERPOOL imetinga Raundi ya Tano ya Kombe la FA baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Bolton Wanderers  hapo jana.

Eidur Gudjohsen aliifungia Bolton bao la kuongoza kwa  mkwaju wa penalti dakika ya 59, baada ya kinda wa miaka 19, Zach Clough kuchezewa vibaya na beki wa Liverpool, Martin Skrtel ndani ya 18

Raheem Sterling akaisawazishia Liverpool dakika ya 85, kabla ya Philippe Coutinho kufunga goli la ushindi dakika ya 90. 

KIUNGO Steven Gerrard amekuwa mchezaji wa tatu wa Liverpool kutimiza mechi 700 kihistoria baada ya kuichezea timu hiyo jana ikishinda 2-1 dhidi ya Bolton katika mechi ya marudio Raundi ya Nne ya Kombe la FA.
Gerrard, ambaye maisha yae yote amecheza Liverpool pekee, alifurahia mafanikio yake hayo kwa kuvaa kiatu maalum kilichoandikwa 700 nyuma pamoja na majina ya mabinti zake, Lilly na Lexie.

Bolton ililazimika kucheza pungufu kwa dakika 20 za mwisho baada ya mchezaji wake, Neil Danns kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na Liverpool sasa itamenyana na Crystal Palace katika Raundi ya Tano.

YANGA YABANIWA NA TFF



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limekataa ombi la Yanga SC kutaka mchezo wao na Mtibwa Sugar uahirishwe ili wapate fursa nzuri ya maandalizi ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF XI ya Botswana.

Na kwa sababu, hiyo Yanga SC wanaondoka asubuhi ya leo kurejea kambini kwao, Bagamoyo kuendelea na maandalizi ya mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Yanga SC watacheza mechi ya tatu ndani ya wiki moja Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya mabingwa wenzao wa zamani wa Ligi Kuu, baada ya Jumapili iliyopita kulazimishwa sare ya 0-0 na Ndanda FC na jana kushinda 1-0 dhidi ya Coastal Union.

Yanga SC ilipanda kileleni mwa Ligi Kuu jana kufuatia ushindi huo wa ugenini, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kwa kutimiza pointi 22 baada ya kucheza mechi 12, moja zaidi ya mabingwa watetezi, Azam FC wanaoshika nafasi ya pili kwa point 21.

Shujaa wa pointi tatu za Yanga SC jana alikuwa ni Nahodha Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’, aliyefunga bao hilo pekee mapema tu kipindi cha kwanza, baada ya kupanda kwenda kusaidia mashambulizi.

Ilikuwa ni dakika ya 12 ya mchezo, wakati Cannavaro alipomalizia kwa kichwa mpira wa kurushwa wa beki Mbuyu Twite na kuipandisha kileleni Yanga SC.

Baada ya mchezo na Mtibwa Sugar Jumapili, Yanga SC itakwenda kuweka kambi visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wa kwanza, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika.
@@@@@@@@@@@@@@@

Wednesday, 4 February 2015

MATOKEO MECHI YA FA MAN UNITED VS CAMBRIGDE UNITED


Na huko Barani ULAYA
KLABU ya Manchester United imetinga Raundi ya Tano ya Kombe la FA baada ya ushindi wa mabao 3-0 Cambridge United Uwanja wa Old Trafford.

Timu ya kocha Mholanzi Louis Van Gaal iliyolazimishwa sare katika mchezo wa kwanza na wapinzani wao hao ugenini, jana ilikuwa tofauti katika mchezo wa pili wa Raundi ya Nne.

Juan Mata alianza kuwafungia bao la kwanza Mashetani Wekundu dakika ya 25, kabla ya Marcos Rojo kufunga la pili dakika ya 32 na James Wilson kumalizia la tatu mnamo dakika ya 73.

Sasa, Man United itasafiri kuwafuata Preston North End katika Raundi ya Tano Jumatatu ya Februari 16, mwaka huu.

Kikosi cha Man Utd jana kilikuwa: De Gea, McNair, Smalling, Evans, Rojo/Young dk81, Blind, Rooney, Di Maria/Herrera dk71, Mata, Van Persie/Wilson dk66 na Fellaini. 

Cambridge Utd: Dunn, Tait, Nelson/Miller dk87, Coulson, Greg Taylor, Donaldson, McGeehan, Champion, Chadwick/Morrissey dk51, Elliott na Simpson/KaiKai dk61. 

YANGA VS COASTAL UNION



 Kilabu ya Dar YOUNG African yenye makazi yake mitaa ya Jangwani imewasili Jijini Tanga tayari kukipiga na coast union katika mchezo wa ligi kuu Vodacom Tanzania bara

Lakini Yanga wamekataa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambao walitakiwa kufanya mazoezi pindi walipofika na kuamua kufanya mazoezi kwenye uwanja wa jeshi.

Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amesema walipanga kufanya mazoezi kwenye uwanja huo na si Mkwakwani.

“Nafikiri hakuna tatizo, kilichotakiwa pale ni suala la mazoezi na tumefanya, hivyo hakuna tatizo lolote,” alisema Muro.

Yanga ipo uwanjani kuvaa na Wagosi wa Kaya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga
Wadau wa soka wanaizungumzia mechi hii ni kama Yanga na SIMBA