C 7 |
Christiano Ronaldo ndiye mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora
Ulaya na Duniani kote maarufu kama Ballon d'Or.
Ronaldo mwenye miaka 29, ametwaa
tuzo hiyo kwa kumbwaga mpinzani wake mkubwa Lionel Messi wa Barcelona na kipa Manuel
Neuer wa Bayern Munich.
Raia huyo wa Ureno ametwaa tuzo hiyo
kwa mara ya pili mfululizo hii ikiwa ni mara yake ya tatu kutwaa tunzo hiyo kwa
kuwa mara ya kwanza aliibeba 2008 akiwa na Manchester United.
Mwaka jana, Ronaldo akiwa na Real
Madrid aliiwezesha kutwaa ubingwa wa Ulaya, Copa del Rey, Uefa Super Cup, pia
ubingwa wa dunia huku yeye akifunga mabao 56 katika mechi 51.
Dakika chache baada ya
kutwaa tuzo ya mchazaji bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amefunguka wazi kwamba
anataka kumfikia mpinzani wake Lionel Messi.
Ronaldo ameeleza
kufurahishwa kwake na kutwaa tuzo yake ya tatu lakini akasisitiza angefurahi
kuichukua kwa mara ya nne kama ilivyo kwa lionel Messi.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako