Tuesday 6 January 2015

HALI YA MCHEZAJI CHRISTOPHER ALEX MASSAWE

Wachezaji wa Simba ambao walishiriki katika kikosi kilichoing’oa Zamalek mwaka 2003 wameamua kumchangia mwenzao Christopher Alex Massawe.
Kikosi cha Simba 2003
 
Massawe yu mgonjwa taabani huko kwao Dodoma. Hali ambayo imewafanya Simba walioifunga Zamalek, Massawe akifunga penalti ya mwisho iliyoihakikishia Simba ushindi.

Kiungo huyo anaumwa na imeelezwa anasumbuliwa na kifua kikuu ingawa bado jambo hilo halijatolewa ufafanuzi na familia yake.

Akizungumza, Boniface Pawasa ambaye alicheza namba tano katika mechi hiyo amesema wanaandaa mechi ya kirafiki ikiwa Lengo ni kupata mechi ambayo itamsaidia ndugu yetu kupata matibabu.

“Wikiendi hii tunaweza kucheza pale Karume kama hakutakuwa na mechi ya daraja la kwanza. Hili ni jukumu letu, wadau wajitokeze.
 
“Tayari baadhi ya waliocheza siku hiyo wamejitokeza, Emmanuel Gabriel na Victor Costa tumeishakubaliana," alisema Boniface Pawasa

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako