Monday 5 January 2015

PANYA ROAD NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM



Vijana 36 wanaodaiwa kuwa ni wa kikundi cha uhalifu kinachojulikana kama PANYA ROAD wanashikiliwa na jeshi la polisi nchini kwa tuhuma za kufanya vitendo vya uhalifu na kuleta hali ya taharuki katika maeneo mbalimbali ya Jiji la DSM hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini DSM, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini ADVERA BULIMBA amesema kwa sasa hali imedhibitiwa na kuwataka Wakazi wa jiji la DSM kuendelea na shughuli zao bila wasiwasi.
Vijana hao wamekuwa na tabia za uporaji wa mali za raia kwa kutumia silaha za mapanga na visu wamekuwa tishio kwa kipindi kirefu jijini Dar es salaam hivyo taarifa za kushikiliwa kwao zimekuwa za faraja kwa watanzania na wakazi wa Dar es salaam kwa ujumla

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako