Sunday 13 April 2014

MZEE GURUMO AFARIKI DUNIA MCHANA WA LEO


Mzee Gurumo afariki dunia leo saa 8:11 mchana katika Hospital ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Taarifa zilizothibitishwa na hospitali ya Taifa Muhimbili zimesema Mzee Gurumo amefariki dunia akiwa hospitalini hapo leo April 13 2014 baada ya kuletwa jana asubuhi na kulazwa kwenye wodi namba 6 ya Mwaisela kutokana na kuzidiwa.

Mwili wa marehemu mzee Gurumo umepelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Muhimbili

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako