Sunday 6 April 2014

DIAMOND KUTUMBUIZA MAREKANI MAY 26 - NDANI YA AYVA CENTER

Yule mkali wa kulishambulia jukwaa Diamond Platiniumz anatarajiwa kufanya bonge la shoo kwenye Ukumbi mkubwa na maarufu wa AYVA Center, ulioko jijini Houston - Texas, Nchini Marekani May 25, 2014.
Ni show kubwa kwa msanii wa Tanzania ambapo kwenye ukumbi huo wameshawai kutumbuiza wasanii wakubwa kama Jay Z, P Diddy, T.I, P Square na wengine wengi.
Mkali huyo wa Ngololo ataongozana na Crew yake ya Wasafi Classic (WCB) kwenda kuwaonyesha jinsi ya kucheza Ngololo watanzania, waafrika na wamarekani wanaopenda muziki wa ki-Tanzania.
Show hiyo itakayokuwa ya kukumbukwa Jumapili hiyo imeandaliwa kwa Ushirikiano wa DMK Global, Safari Entertainment na J & P Entertainment.
Diamond anatarajiwa kurudi tena Nchini Marekani July 26, 2014 kuhudhuria Tuzo za AFRIMMA Awards 2014 akiwa na wasanii mbalimbali kutoka kila kona ya Dunia, akiwemo Fally Pupa, Wyre, Davido, 2 Face, T-pain, Flavour.
 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako