Sunday 13 April 2014

MAKAMU WA RAIS, MKUU WA MKOA, NA WAZIRI MAGUFURI WANUSURIKA KATIKA AJALI YA HELIKOPTA


Helkopta ya Polisi yapata ajali muda mchache baada ya kuruka katika Uwanja wa Ndege asubuhi ya leo.
Imeafiriwa kuwa, viongozi watatu wa Serikali, Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki wamenusurika katika ajali ya helikopita ya Jeshi iliyotokea leo jijini Dar es Salaam walipokuwa wakijiandaa kuelekea kukagua maafa yaliyosababishwa na mafuriko ya mvua zinazoendelea kunyesha kote nchini.
Hata hivyo, taarifa za mtu ambaye hakutaka kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa Jeshi la Polisi amesema, kuwa hakuna kiongozi aliyeripotiwa kujeruhiwa sana na hivyo Dk Bilal aliazimu na kuendelea na ziara ya ukaguzi kwa kutumia gari

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako