Klabu ya Dar Young African yenye makazi yake Jangwani Jijini Dar
es salaam imelazimishwa sare ya goli 2 kwa 2 na Wana Lamba lamba Azam Fc katika
uwanja wa Taifa hapo jana
Clab ya Azam ilikuwa ya kwanza kuona lango la Yanga mnamo dakika
ya 6 pale Mbuyu Twite alipojichanganya na kipa wake Dida na kumpa nafasi Didier
Kavumbagu kuamsha mashabiki wa Azam kwa shangwe
Lakin punde si punde furaha hizo zikazimwa na wana jangwani hao
baada ya aliyekuwa mchezaji wa kulipwa wa simba Hamis Tambwe Hamis Magoli
kutupia bao zuri la kichwa mnamo dakika ya 7
Mpaka muda wa mapumziko timu hizo zilikuwa zimetoshana nguvu kwa
goli kwa moja
Na kufanya mchezo kuwa wakuvutia zaidi pale tulipoona usajili wa
mashabiki na mbwembwe zao uwanjani
Mnamo dk ya 52 Simon Msuva wa Yanga aliiandikia timu yake bao la
pili na kuifanya Dar Yang AFRICAN kutawala mchezo huo, hadi ambapo
Azam waliamka na kufanya mabadiliko mnamo dakika ya 64 bada ya
kumtoa Salum Abubakar sure boy na kumwingiza Nahodha Jon Bocco Adebayo ambae
hakufanya makosa mnamo dakika ya 65 alitupia mpira wa kichwa matata uliomshinda
kipa shaban Dida na kutinga wavuni
Katika mechi hiyo timu ya Yanga iliwachezesha wachezaji wake
wageni huku ikiwa ni mechi ya kwanza kwa kocha mpya Hans Van de pluijm
Yanga sasa inajiandaa kuumana na Mbeya City kwenye Uwanja wa
Sokoine kisha kuivaa timu ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.