Monday 15 December 2014

KISA CHA MAJOGOO YA ENGLAND KULALA KWA MASHETANI MEKUNDU

Kilabu ya Manchester United imeicharaza Liverpool mabao matatu bila majibu katika mechi ya kasi iliojaa mashambulizi makali kutoka pande zote mbili.
Hata hivyo ni Manchester United ndio walioona lango la Liverpool kupitia bao la nahodha wao Wayne Rooney katika kipindi cha kwanza cha mchezo
Yuan Mata alifanya mambo kuwa mbili bila baada ya kufunga krosi iliopigwa na Young,bao ambalo wachezaji wa Liverpool walidhani ni la kuotea.

lakini Licha ya Liverpool kunoa safu yao ya mashambulizi na kuvamia ngome ya Manchester United kupitia Sterling aliyekosa mabao ya wazi Manchester united iliendelea kufanya mashambulizi kupitia Van Persie na Rooney.
Liverpool ilimuingiza Mario Balotelli ambaye pia naye alikosa mabao ya wazi huku Kipa wa Manchester akinyaka mashambulizi hayo.

Na baada ya dakika kadhaa Robin Van Persie alifanya mambo kuwa 3-0 baada ya safu ya ulinzi ya Liverpool kufanya masihara katika lango lao.
Liverpool sasa inajiandaa na mechi dhidi ya Arsenal katika mchezo unaofuata.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako