LIVERPOOL PLAYER COUTINHO |
Kocha wa
Liverpool, Jurgen Klopp amesema ushangiliaji wake pamoja na wachezaji wa
Liverpool baada ya ushindi dhidi ya arsenal hauruhusiwi.
Katika
mchezo wa ligi kuu ya england uliochezwa jioni ya jana jijini London, wenyeji
wa emirates arsenal waliangukia pua baada ya kupata kipigo cha magoli 4-3
kutoka kwa majogoo wa anfield Liverpool.
Liverpool
iliyochini ya klopp imeanza kampeni ya kusaka ubingwa wa epl kwa ushindi mnono
licha ya arsenal kutangulia kufunga katika kipindi kwanza kupitia kwa goli
lililofungwa na theo Walcott katika dakika ya 31 lakini kabla kipenga cha
mwamuzi kupulizwa kuashiria kipindi cha kwanza kumalizika philipe coutinho
aliisawazishia Liverpool kupitia mkwaju wa mpira wa adhabu ulizama wavuni
katika dakika ya 45.
Katika
kipindi cha pili Liverpool waliongeza idadi ya magoli dhidi ya wapinzani wao
ambapo katika dakika ya 49 adam lallana aliukwamisha mpira wavuni kabla ya
coutinho kurejea tena wavuni katika dakika ya 56 na saido mane kushindilia
msumari wan ne katika dakika ya 63.
Arsenal
walikusanya nguvu na dakika moja baada ya goli la mane, alex oxlade chamberlane
aliifungia arsenal goli safi akiivuruga safu ya ushambuliaji ya Liverpool na
calum chambers akifunga la tatu katika dakika ya 75.
“sikupaswa kushangilia goli la
nne wakati ilibaki nusu saa nzima. Nilifahamu kwa wakati ule lakini
nilishachelewa”.
Aidha klopp
amesema kilichomfurahisha zaidi katika ushindi huo ni namna ambavyo walitulia
na kujilinda katika kipindi cha dakika 30 za mwisho ambapo arsenal walizidisha
mashambulizi na hata kupelekea kuonekana huenda isingekuwa siku yao kushinda.
Upande wa
pili wa shilingi mambo si shwari kwa kocha wa arsenal arsene wenger ambaye
kikosi chake kinazidi kuandamwa na majeruhi.
Pamoja na kipigo cha ufunguzi asrenal imepata pigo la majeruhi baada ya
mshambuliaji kinda wa timu hiyo alex iwobi kupata majeraha sambamba na kiungo
aaron ramsey ambao walilazimika kutolewa nje kabla ya mechi kumalizika.
Kwa upande
wake Kocha wa Manchester united Jose Mourinho ameelezea kufurahishwa na kiwango
alichokionyesha kiungo Juan mata baada ya kufunga goli katika mchezo wao dhidi
ya Bournemouth.
Mata
alifungua ukurasa wa magoli wa united msimu huu baada ya kupachika goli dakika
5 kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika na kuipa uongozi united katika dimba
la vitality, kabla ya wayne rooney na Zlatan Ibrahimovic kuongea mengine mawili
katika kipindi cha pili.
Adam Smith
aliifungia Bournemouth goli la pekee lakini kikosi hicho cha mourinho kilipigana
kuwazuia Bournemouth kuongeza mengine mpaka mpira kumalizika na kujinyakulia
pointi tatu muhimu.
Mata ambaye
aliuzwa united na mourinho alipokuwa Chelsea alifanyiwa mabadiliko ya kutolewa
nje baada ya kuingia uwanjani katika mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Leicester
na sakata hilo kuleta mtazamo tofauti baina ya mashabiki wa united lakini
mourinho ni kama aliwajibu mashabiki hao kwamba hakuna kitu yao na kuamua
kumuanzisha mata katika mchezo wa jana na mourinho kusema ilikuwa mechi sahihi
kwa mata kuonyesha kiwango chake.
“lilikuwa goli muhimu lenye kutumia akili, goli kutoka kwa mtu wa mpira.
Namjua vizuri kwasababu nimefanya nae kazi kwa miezi sita tulipokuwa Chelsea,
najua fika kipi anachoweza kutoa na kipi asichoweza”.
Mourinho ameongeza kuwa anafuraha kwa mata
lakini pia anafuraha kwa timu nzima hata wale waliokuwa nje na kuingia kutoa
mchango wao katika ushindi na hata wasiopata nafasi ya kucheza kwani wote kwa
pamoja wanajenga familia moja.
Mechi
inayofuata united watawakaribisha Southampton old Trafford na mourinho kuwa na
mtazamo chanya kuelekea mchezo huo hasa baada ya kupata ushindi mfululizo.
@@@@@@@@@@@@@
Nae kocha
wa Manchester city, pep guardiola amekiri kwa mlinda mlango wake joe hart
kuchukizwa kwa kuachwa katika kikosi cha man city wakati timu hiyo ikianza
mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi wa ligi kuu ya epl.
Mara baada
ya kuteuliwa kuwa kocha mpya wa timu hiyo, guardiola hakuchelewa kubadilisha
baadhi ya vitu ikiwa ni sambamba na kumuacha mlinda mlango huyo ambaye si tu
chaguo la kwanza kwa klabu ya man city lakini pia ni mlinda mlango nambari moja
wa timu ya taifa ya England.
Hart
aliishuhudia timu yake siku ya jumamosi ikishinda magoli 2-1 dhidi ya
sunderland akiwa nje na kitendo hicho kuibua tetesi za mlinda mlango huyo
kutimka city.
Guardiola
amesema ana uhakika kwamba hart amechukia, lakini si kila mchezaji asiyepata
nafasi katika kikosi kitakachoanza atauzwa bali amesema kuwa anatakiwa achague
timu na kwa sasa ana wachezaji 28 na kati ya hao wanatakiwa wamshawishi zaidi
uwanjani.
Licha ya
kuwa na msimu mzuri 2015/2016 na kuwa mchezaji muhimu wa man city katika miaka
ya hivi karibuni lakini kushindwa kuonyesha makali katika michuano ya kimataifa
ya euro mwaka kumeifanya klabu ya man city kuhusishwa na kutaka kusajili
magolikipa wengine huku taarifa hizo zikichagizwa zaidi na ujio wa pep
guardiola.
Hata hivyo
guardiola ametupilia mbali taarifa za kumshusha hart na kusema bado mlinda
mlango huyo anaweza kuwa chaguo lake la kwanza na kutetea uamuzi wake wa
kumuanzisha langoni willy caballero kwani muarjentina huyo alianza mazoezi
mapema kabla ya joe hart.
@@@@@@@@@@@@@@@