Monday, 1 July 2013

BRAZIL ILIVYOISAMBARATISHA SPAIN KWA MABAO 3-0


MAGOLI yaliyofungwa na mshambuliaji Fred wa Fluminence na Neymar yalitosha kuipa brazil ushind wa mabao 3-0, na kutangazwa kuwa mabingwa wa kombe la shirikisho katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa  Maracana uliopo nchini brazil.
Ilichukua dakika mbili tu kwa mshambuliaji  Fred wa Brazil kukwamisha wavuni bao la kwanza mara baada ya kutokea kuzembea kwa mabeki kuhamisha mpira eneo la hatari la Spain na kuiandikia Brazil bao la kwanza.
Neymar aliifungia Brazil bao la pili dakika chache kabla ya kwenda mapumziko kwa kiki kali ya mguu wa kushoto akipokea pasi toka kwa Oscar na kuiandikia Brazil bao la pili kabla ya Fred kufunga bao la tatu dakika za mwanzo za kipindi cha pili.
Katika mchezo huo mchezaji wa Spain Sergio Ramos alikosa penat dakika ya 50 ya kipindi cha pili mara baada ya Marcelo kumkwatua Jesus Navas katika eneo la hatari.
Dakika ya 68 mchezaji Gerald Pique alitolewa nje kwa kadi nyekundu mara baada ya kumchezea faulo MCHEZAJI Neymar wa Brazil na hadi mpira unamalizika Brazil 3-0 Spain.
MKALI WA MABAO NEYMAR ALIKUWA MIONGONI MWA WACHEZAJI WALIOCHEZEWA FAULU NYINGI KATIKA MCHEZO HUO
WACHEZAJI WA BRAZIL WAKIMPONGEZA NEYMAR BAADA YA KUFUNGA MIONGONI  MWA MAGOLI YAKE KATIKA MCHEZO HUO WA FAINALI
BRAZIL WAKISHEREHEKEA MARA BAADA  YA KUKABIZIWA KOMBE LAO
MUUAJI NEYMAR AKISHANGILIA BAO  LA PILI KATIKA MCHEZO HUO
MUUAJI WEA  KIBRAZIL FRED AKISHANGILIA BAO LA KWANZA ALILOWAFUNGA SPAIN MNAMO DAKIKA YA PILI
FRED AKISUMBUA NGOME YA WAISPANIOLA HUKU AKIZUIWA NA AZPALCUETA WA SPAIN

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako