Monday 29 December 2014

MECHI YA AZAM NA YANGA


Klabu ya Dar Young African yenye makazi yake Jangwani Jijini Dar es salaam imelazimishwa sare ya goli 2 kwa 2 na Wana Lamba lamba Azam Fc katika uwanja wa Taifa hapo jana

Clab ya Azam ilikuwa ya kwanza kuona lango la Yanga mnamo dakika ya 6 pale Mbuyu Twite alipojichanganya na kipa wake Dida na kumpa nafasi Didier Kavumbagu kuamsha mashabiki wa Azam kwa shangwe
Lakin punde si punde furaha hizo zikazimwa na wana jangwani hao baada ya aliyekuwa mchezaji wa kulipwa wa simba Hamis Tambwe Hamis Magoli kutupia bao zuri la kichwa mnamo dakika ya 7
Mpaka muda wa mapumziko timu hizo zilikuwa zimetoshana nguvu kwa goli kwa moja
Na kufanya mchezo kuwa wakuvutia zaidi pale tulipoona usajili wa mashabiki na mbwembwe zao uwanjani

Mnamo dk ya 52 Simon Msuva wa Yanga aliiandikia timu yake bao la pili na kuifanya Dar Yang AFRICAN kutawala mchezo huo, hadi ambapo
Azam waliamka na kufanya mabadiliko mnamo dakika ya 64 bada ya kumtoa Salum Abubakar sure boy na kumwingiza Nahodha Jon Bocco Adebayo ambae hakufanya makosa mnamo dakika ya 65 alitupia mpira wa kichwa matata uliomshinda kipa shaban Dida na kutinga wavuni

Katika mechi hiyo timu ya Yanga iliwachezesha wachezaji wake wageni huku ikiwa ni mechi ya kwanza kwa kocha mpya Hans Van de pluijm

Yanga sasa inajiandaa kuumana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine kisha kuivaa timu ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.


No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako