Saturday 22 February 2014

AY AZIDI KUTENGENEZA FEDHA ZAIDI KUPITIA MATANGAZO


Diamond Platniumz na Mzee wa Commercial, walionekana kwenye ndege hivi karibuni wakielekea Nchini Afrika Kusini, Taarifa zinasema ya kuwa  wamekwenda kwa ajili ya video ya One Campaign inayohusisha wasanii zaidi ya 20 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Baada tu ya kutua ndani ya ardhi ya Tanzania ameingia tena kwenye vichwa vya habari kupitia   tangazo la Television la Kampuni ya vitu tofauti ya Samsung.

Ay Alipost Hii Picha akiwa na mwanamitindo Zuu maarufu kama Zuu wa Kamiligado kisha akaweka  ujumbe huu.
“Team no sleep…Mzee wa Commercial on Set.. #SAMSUNGNEWTVC”

HUYU NDIYE MSICHANA ANAYEDAIWA KUWAAMBUKIZA ‘NGOMA’ MASTAA NCHINI KENYA


Kupitia mtandao wa Kenyan Post, hivi karibuni walipost stori ya mwanadada mwenye umri wa miaka 16 ambaye aitwaye Vanesa Chettle ilidaiwa kuwa ni mwathirika wa ugonjwa wa Ukwimwi na amekuwa akiwaambukiza kwa makusudi mastaa wa nchini humo
Msichana huyo inasemekana ameshafanya mapenzi na watangazaji wa kituo kimoja cha radio ambao ni Shafie Weru na Nick Mutuma, pia ameshafanya mapenzi na mwigizaji Effy, na sasa mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 16 anaishi na kibabu cha Kizungu chenye cha umri wa miaka 80, pia inasemekana Vanesa ameshapiga ‘group sex’ na Top Kenya n deejays kwenye pati.
Inasemekana kuwa msichana huyo ni mcheshi na mtundu sana uwanjani, inadaiwa kuwa ameshatembea na waume za watu na mara kibao amekamatwa na polisi lakini huyo babu wa kizungu tajiri anayeishi naye huwa anawapa mitonyo polisi na kumtoa

NEXT STEP YA DIAMOND PLANTINUMZ


Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz bado anaendelea kuudhihirishia ulimwengu kwamba anapiga hatua kulingana na juhudi alizonazo kwenye muziki, hili ni shavu lingine, kwa sasa Diamond ameteuliwa kuwa moja kati ya wasanii wanaootoka Afrika na watakaoshiriki katika Tuzo za muziki zitakazofanyika huko Eisemann Center Dallas Nchini Marekani.
Tuzo hizi zinatarajiwa kufanyika July 26 2014 na pia inategemewa kuwakutanisha wasanii mbalimbali kutoka Africa Magharibi Kusini na sehemu zingine na taarifa iliyopo ni kwamba Mc wa shughuli hiyo atakuwa ni mchekeshaji kutoka Nigeria Basket Mouth pamoja na Na Mrembo Pia Muigizaji Kutoka Nollywood Juliet Ibrahim
Show hiyo inategemewa kuanza saa 2 kamili usiku na hii ni miongoni mwa show kubwa kwa wa Africa maana Itakusanya wadau kibao wa muziki wa kiafrika Duniani kutakua na Wanamuziki,Ma producer,Ma Manager,Dj’s Na kila anaeendeleza Tamaduni za Kiafrica.
Unaambiwa pia Wageni kutoka Mataifa 17 ya Africa wanatarajia kutoka Miji ya mbali mbali ya Nchini Marekani kuhudhuria Tuzo Hizo Ambapo kwa hapa Tanzania tunatarajia kuwakilishwa na Diamond Platinumz.
Diamond pia wiki chache zilizopopita alitoa Sample ya ClothingLine yake yenye nembo ya Wasafi Classic Baby.

WALINZI WA USALAMA 70,000 WAONGEZWA BRAZIL KUHAKIKISHA AMANI KWENYE MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA


Brazil imetangaza kwamba wameongeza maafisa wa kulinda usalama 70,000 zaidi watakaotoa huduma za usalama katika fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.
Idadi hii iliyoongezwa ni katika jitihada za kukabiliana na tishio la usalama na maandamano.
Idadi iliyopendekezwa hapo mbeleni ya maafisa 100,000.
Kwa ujumla maafisa wa usalama wapatao 170,000 watatumika katika miji 12 itakayoandaa mashindano hayo.
Jumatano wiki hii Rais wa Brazil Dilma Rouseff alisema kwamba jeshi litajumuishwa kwenye mpango huo dhabiti wa usalama iwapo kutaibuka wimbi lingine la maandamano.
Hatua hii inafuatia visa vya ghasia zilizoshuhudiwa katika miji tofauti tangu mwezi Juni mwaka uliyopita wakati Brazil ilipoandaa mchuano wa Kombe la Mashirika.
Mkuu wa Usalama wa Shrikisho la Soka Duniani FIFA amesema kuwa ana uhakika kwamba Brazil itaandaa michuano wenye usalama.
Kati ya idadi hiyo ya maafisa wa usalama, 150,000 watachaguliwa kutoka katika vikosi vya Polisi na mashirika mengine ya usalama huku wengine 20,000 watatoa huduma usalama ndani ya viwanja vyote 12.
Vikosi vya jeshi la wanamaji pia litazindua mazoezi ya kwanza kwa matayarisho ya dimba la Kombe la Dunia.
Operesheni hiyo maalum ya kupambana na ghasia inawahusisha wanajeshi 20,000, meli 60 na ndege 15 za kivita

Friday 21 February 2014

PICHA ZA BIRTHDAY YA RIHHANA JANA

ROBERT MUGABE ATIMIZA UMRI WA MIAKA 90, FAHAMU MAMBO 9 USIYOYAJUA


Alizaliwa katika kijiji cha Kutama, Kusini-Magharibi mwa jiji kuu Harare, alisomeshwa na Wayesuti, na baadaye akawa mwalimu kabla kujiingiza katika harakati za kupigania uhuru wa Zimbabwe.
Uwanaharakati wake ulimfanya afungwe gerezani kwa miaka 11, na baadaye mwaka 1980 akawa rais wa kwanza wa Zimbabwe.
Yafuatayo ni mambo tisa ambayo huenda hukuwa wayajua kumhusu kiongozi huyu na ambayo huenda yamemuwezesha kuwa rais kwa muda mrefu mno.
1) Zoezi na vyakula vya kienyeji
Mugabe anapenda kufanya mazoezi. “Mimi hujihisi mgonjwa wakati sijafanya mazoezi ya viungo vya mwili,” Bw. Mugabe alisema miaka mitatu iliyopita. Huwa anaamka kati ya saa kumi na kumi na moja alfajiri, na kutokana na jamaa zake wa karibu, husikiliza BBC idhaa ya dunia.
Siri nyingine ya kuishi kwake kwa muda mrefu ni kuwa hupenda sana-chakula cha kienyeji kinacholiwa sana Zimbabwe. Kisha pia, havuti sigara, ila hunywa pombe kidogo anapokula.
2) 'Kufufuka'
Ingawa kumekuwa na uvumi mara nyingi kuwa Mugabe hana afya nzuri, afya yake na kazi yake ya kisiasa yaendelea vyema kabisa. Kuhusu afya yake Mugabe alipohojiwa wakati mmoja alisema,“ Nimekufa mara nyingi-hapo ndipo humwelekea Yesu Kristo. Yesu alikufa mara moja, na akafufuka mara moja,” alisema alipotimia miaka 88.
Ingawa alilelewa katika familia ya kikatoliki mamake alikuwa mcha Mungu alisema alipohojiwa na kituo cha habari cha Afrika Kusini, SABC  miaka michache iliyopita, kuwa yeye si Mkristo anayetumikia dini kwa sana.
3) Shabiki mkubwa sana wa kriketi
Kwa muda mrefu amedhihirisha hadharani mapenzi ya mchezo wa kriketi. Ni patroni wa jumuiya ya mchezo wa kriketi wa Zimbabwe, ambapo nyumba yake ipo karibu na uwanja wa michezo wa Harare, ambapo anaweza kutazama kwa makini wakati wa michezo wa kitaifa.
“Kriketi yafanya watu wawe wangwana, na pia inawafanya watu kuwa wema,” Bw. Mugabe alisema miaka kadhaa baada ya Zimbabwe kujinyakulia uhuru. “Nataka kila mtu acheze kriketi Zimbabwe; nataka nchi ya Zimbabwe iwe nchi ya wangwana.”
4) Hapendi kushindwa
Alipokuwa kijana, Mugabe alikuwa mmakinifu na mzuri kabisa katika mchezo wa tennis,” alisema aliyekuwa mwalimu katika shule ya Wakatoliki alikosomea Mugabe.  Ila aliposhindwa katika mchezo huo, aliitupa raketi yake chini kwa hasira.
Mugabe amekiri kuwa hakuwa mzuri katika mchezo wa kandanda alipokuwa mdogo, ila kwa sasa, anapenda kuutazama mchezo huo.
Yeye ni shabiki wa vilabu vya Chelsea na Barcelona vilivyoko Uingereza na Uhispania mtawalia. “ Ninapotazama kandanda, sitaki usumbufu kutoka kwa mtu yeyote,” alisema mwaka wa 2012. “Hata mke wangu anajua mahala pa kukaa wakati wanapofunga bao uwanjani, hata mimi pia hufunga bao kwangu kwa kupiga mateke vitu vyovyote vilivyoko mbele yangu.”
5) Alipata mtoto akiwa miaka 73
Ana watoto watatu na mke wake wa pili, Grace Marufu, aliyekuwa karani wake. Mtoto wao wa tatu alizaliwa 1997, mwaka mmoja baada ya wao kufunga ndoa.
Mwanawe wa kwanza, Nhamodzenyika, alikufa kutokana na Malaria akiwa miaka mitatu bado wakiwa Ghana. Bw. Mugabe alinyimwa ruhusa ya kuenda Accra kuungana na mkewe kwa mazishi ya mwanawe, kwani alikuwa mfungwa wa kisiasa wa serikali ya enzi hiyo ya Rhodesia.
6) Anampenda Cliff Richard kuliko Bob Marley
Mwanasiasa wa Zimbabwe ambaye kwa sasa ni hayati, Edgar Tekere, alimwambia mwandishi wa BBC, Brian Hungwe, kuwa alipokuwa akitayarisha kadhia ya kusherehekea uhuru wa Zimbabwe 1980, Bw. Mugabe hakumtaka muimbaji Bob Marley aalikwe kutumbuiza watu, ila alimtaka muimbaji maarufu wa Uingereza, Cliff Richard. Pia anampenda Muimbaji, Jim Reeves.
Mugabe anawachukia sana wanamitindo wa rasta, na waimbaji wa mitindo ya reggae. Aliwaonya vijana wa Zimbabwe: “ Nchini Jamaica, wanauhuru wa kutumia bhangi, na wanaume huwa wakati wote wamelewa. Hawataki kuenda shule; wanataka tu kuimba, na kufuga rasta. Kama Zimbabwe, tusielekee hapo.”
7) Mvaaji wa nguo maridadi
Anapenda sana suti zinazoutosha mwili wake kisawasawa na tai zinazofanana na kitambaa. Huwavutia sana wanamitindo nchini Zimbabwe kwa mavazi yake. Ila, mwanamitindo ambaye humshonea nguo zake, Khalil Parbhoo anasema: “Bado huvaa kama mabwana wa Uingereza –hivyo ndivyo anavyopenda."
8) Anamtazama Kwame Nkrumah kama kielelezo kwake
Taarifa kuhusu hali ya kiafya ya Mugabe zimekuwa zikigonga vichwa vya habari karibuni
Bw. Mugabe alipata azma ya siasa akiwa Ghana alipokuwa mwalimu; mahali alipokutana na mke wake wa kwanza, Sally Hayfron.
Aliporudi Zimbabwe, aliwaambia wananchi jinsi Ghana ilivyojinyakulia uhuru na jinsi uhuru ni kitu kizuri. Katika mahojiano mwaka 2003, Mugabe alisema: “Niliwaambia pia kuhusu Kwame Nkrumah jinsi alivyojitolea na kuiongoza Ghana kupata uhuru; Kwame aliwaambia wananchi wa Ghana kuwa Ghana haingekuwa nchi huru bila ya jitihada na kujitolea kwa kila mtu.”
9) Ni mtu mwenye shahada nyingi
Kwa jumla, Mugabe ana shahada saba. Digrii yake ya kwanza ni kutoka katika chuo kikuu cha Fort Hare kilichoko Afrika Kusini. Alisomea digrii zake zingine kwa njia Internet-mbili akiwa gerezani-shahada hizo ni za: elimu, sayansi, sheria na usimamizi.
Amejitapa kuwa na “shahada katika ujuhula” alipokuwa akivionya vyama vya kutetea haki za wafanyakazi nchini Zimbabwe 1998 kila vilipotishia kugoma.

P FUNK "MAJANI" AZURU KABURI LA MANGWAIR MOROGORO

" Visit Ngwair's Grave on my way back from Dodoma, It was Very Emotional" Aliandika P Funk

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YATANGAZWA, UFAULU WAPANDA 2013

Matokeo ya Kidato cha nne 2013 yatangazwa, kiwango cha ufaulu chapanda kwa asilimia 15.17 kutoka asilimia 43.08 mwaka 2012 hadi 58.25 mwaka 2013.
Watahiniwa wafaulu zaidi katika somo la Kiswahili (67.77%), na wafanya vibaya zaidi Basic Mathematics (17.78%)
ST. FRANCIS SHULE YA WASICHANA YAONGOZA TANZANIA NZIMA KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YAWA YA KWANZA

DIV-I = 81 DIV-II = 8 DIV-III = 1 DIV-IV = 0 DIV-0 = 0

DIAMOND NA AY WAPATA SHAVU AFRIKA KUSINI


Siku chache kupitia mitandao ya kijamii mbalimbali kama Instagram,Facebook na Twitter, Diamond Platnumz amekua akipost picha nyingi akiwa nchiniAfrika kusini na wasanii mbalimbali wa Afrika akiwemo Dbanji.
Maswali yalikuwa mengi kichwani na mara nyingi tunaamini wasanii wanapokutana pengine wana mipango ya kushirikiana kwenye kazi za kisanii ama wana ukaribu mkubwa unaowafanya kuwa pamoja.

Blog hii imefuatilia na kugundua safari ya Diamond South Africa ni moja kati ya miradi ya One Campaign na hii ya sasa ni kupitia mradi wake wa Go Agric ambapo inahusu kufanya video na wimbo wa pamoja na zaidi ya wasanii 20 wa Afrika.

Video tayari imefanyika Johannesburg Afrika Kusini kwenye studio za M1 zinazomilikiwa na shirika la SABC, kwa Tanzania wasanii waliowakilisha ni AY na Diamond, wasanii wengine waliopo kwenye mradi huo ni pamoja na D’Banj, Femi Kuti wa Nigeria, Victoria Kimani wa Kenya na wengine.

LEO IJUMAA NDANI YA MAISHA CLUB, VIDEO ZA WANAIJA UTAKOSAJE!!!!!!


SAKATA LA KUONGEZEWA POSHO KWA WABUNGE WA KATIBA, ZITO AKATAA NYONGEZA

 

FACEBOOK YANUNUA APLICATION YA WHATSAPP KWA DOLA BILION 19


Facebook wanazidi kujitanua zaidi kibiashara katika ulimwengu huu wa dijiti ambapo wameweza kufanya makubalino na waanzilishi wa ‘WhatsApp’, Jan Koum na Brian Acton kuinunua kwa makubaliano ya jumla ya dola bilioni 19 pamoja na hisa.

Mwanzilisihi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa walianza kuzungumzia hatua hiyo siku 11 zilizopita ili waweze kuimiliki WhatsApp ambayo hivi sasa inawatumiaji zaidi ya milioni 450 kwa mwezi.

Mwanzilishi wa WhatsApp ambaye alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya Yahoo!, Jan Koum ameonesha kulifurahia deal hilo na kudai kuwa ni heshima kwao kwa kuwa mbali na pesa watakazolipwa, yeye pia atakuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Facebook.

“We’re excited and honoured to patner with Mark and Facebook as we continue to bring our product to more people around the world.” Alisema Jan Koum.
Ingawa mmiliki wa Facebook anaamini kwamba kwa kutumia WhatsApp wataweza kuwavuta mabilioni ya watumiaji, amesisitiza kuwa hana mpango wa kuweka matangazo kwenye mfumo huo na kwamba hadhani kama kuweka matangazo kwenye mfumo wa kutuma ujumbe ni njia bora zaidi ya kutengeneza pesa.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Facebook italipa fedha taslim dola bilioni 4 na kiasi cha hisa zake kinachokadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 12, na ziada ya dola bilioni 3 zitakazolipwa baadae.
Deal hilo litakapokamilika na wakalipwa kiasi hicho, waanzilishi wa WhatsApp Jan Koum na Brian Acton wanatarajiwa kutangazwa kuwa mabilionea wapya.

Kampuni ya WhatsApp Inc. ilianzishwa mwaka 2009 na watu wawili waliokuwa wafanyakazi wa kampuni ya Yahoo, mmarekani Brian Acton na raia wa Ukrain Jan Koum, ambapo wanadai kuwa kwa hivi sasa huwasajili watumiaji wapya milioni moja kwa siku.
Ikumbukwe ya kuwa mwaka May, 2009 Brian Acton alipeleka maombi ya kazi katika kampuni ya Facebook pamoja na Twitter lakini maombi yake ya kazi yalikataliwa na hivyo akarudi mtaani na kujipanga ambapo waliungana na Jan Koum kuanzisha WhatsApp.