OMMY DIMPOZ AENDELEA KUFANYA KWELI
Ni zamu ya staa wa bongofleva anayetajwa kuwa
wa pili kwa kupokea malipo makubwa kwenye show mbalimbali anazozifanya (milioni
nane kwa show za ndani ya nchi).
Siku kadhaa baada ya kutua Tanzania akitokea
Marekani na Uingereza alikokwenda kufanya show pia, Ommy Dimpoz amepata dili
jingine zuri kwa kualikwa kuimba na band yake aliyotoka nayo bongo katika party
ya kampuni ya mafuta huko Muscat Oman.
Kwa siku kadhaa Ommy ambae ni miongoni mwa
vijana wachache wa bongofleva wanaosifika kwa kujituma na kuwa serious na kazi,
alionekana akifanya mazoezi na band yake ambayo ndio atahusika nayo mwanzo
mwisho kwenye stage Leo Ijumaa March 28 2014
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako