Kocha wa zamani wa Barcelona, Pep
Guardiola, leo hii ameifunga timu hiyo ambao ndio mabingwa wa La Liga kwa jumla
ya mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika huko Munich.
Philipp Lahm ndie aliyeanza kuingiza
mpira nyavuni katika kipindi cha kwanza katika dakika ya 14,
na Mario Mandzukic akaipatia Bayern bao la pili dakika ya 87. Barcelona ilikuwa ikiongozwa na Jordi
Roura, wakiwa bado wanamsubiri kocha wao mpya Gerardo Martino, walishindwa
kutoka na ushindi katika mchezo huo, huku Messi akibadilishwa na Dongou.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako